Paris,Ufaransa.
ILE shauku ya kutaka kujua kuwa,Hatem Ben Arfa, atajiunga na timu gani, tayari kwa msimu ujao wa ligi za Ulaya hatimaye leo imefikia mwisho baada ya winga huyo wa zamani wa Newcastle United aliyekuwa akiwindwa na vilabu zaidi ya 13 kujiunga na Paris Saint-Germain kwa mkataba wa miaka miwili.
Ben Arfa,29,ametua Paris Saint-Germain akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja katika iliyokuwa timu yake ya zamani,OGC Nice.
Akiwa na OGC Nice msimu uliopita, Ben Arfa alifunga mabao 18 na kutengeneza mengine sita katika michezo 35 hali iliyofanya vilabu kama Liverpool,Barcelona,Sevilla kuanza kummendea kwa lengo la kutaka kumsajili.
Ben Arfa amepewa jezi namba 21 ambayo iliwahi kuvaliwa na Lucas Digne,Marquinhos pamoja na nyota wa zamani wa dunia,Mbrazil Ronaldinho Gaucho.
0 comments:
Post a Comment