Christian Kabasele
Allardyce:Meneja wa zamani wa Manchester United,Sir Alex Ferguson,amepanga kukiambia cha soka cha England FA kumteua,Sam Allardyce, kuwa Meneja mpya wa timu yake ya taifa kwa kuwa Meneja huyo wa Sunderland ameshafanya mengi na ana uzoefu mkubwa katika kufundisha soka.(The Sun)
Takuma:Meneja wa Arsenal,Arsene Wenger ana matumaini makubwa kuwa mapema wiki ijayo atakamilisha usajili wa mshambuliaji wa Japan,Takuma Asano,21,kutoka Sanfree Hiroshima na kisha kumtoa kwa mkopo ili apate uzoefu wa kucheza soka barani Ulaya kabla ya kuamua kumtumia katika kikosi chake.(Daily Mail)
Mourinho Jr:Mtoto wa Meneja wa Manchester Unuted,aitwaje Jose Mario Mourinho Jr amejiunga na shule ya soka inayomilikiwa na Fulham kwa mkataba wa miaka miwili.Mourinho Jr anacheza nafasi ya ulinda mlango.(Goal)
Mandanda:Crystal Palace imekiongezea nguvu kikosi chake baada ya leo hii kumsajili mlinda mlango wa Ufaransa,Steve Mandanda,31,toka Marseille kwa mkataba wa miaka mitatu.Pia imemsajili winga Andros Townsend,24,toka Newcastle United kwa mkataba wa miaka mitano kwa ada ya £13m.(The Sun)
Vieira:Leicester City imefungua mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Gremio,Luan Vieira ili kuangalia uwezekano wa kumsajili staa huyo mwenye thamani ya £20m.(ESPN Brasil)
Peres:Manchester City italazimika kujikamua zaidi ili kuweza kuinasa saini ya mlinzi wa kulia wa Torino,Bruno Peres,hii ni baada ya ofa yake ya awali ya £12.4m kukataliwa na miamba hiyo ya Italia. (Gazzetta dello Sport)
Seaman:Mlinda mlango wa zamani wa Arsenal,David Seaman,amesema meneja wa klabu hiyo Mfaransa,Arsene Wenger,66, siyo mtu sahihi wa kuchukua kibarua cha kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya England.(Daily Mail)
Kante:Kiungo wa Ufaransa,N’Golo Kante,25,ameripotiwa kujiandaa kukataa mkataba mpya wa kuendelea kubakia Leicester City ili aweze kujiunga na Chelsea.(Daily Teregraph)
Koscielny:Baada ya Bayern Munich kuanza kumfukuzia kwa mara ya pili mlinzi wa Ufaransa,Laurent Koscielny,30,amemeripotiwa kutaka kutumia mwaya huo kuitaka Arsenal impe ongezeko la mshahara mpaka kufikia £90,000 kwa wiki.(Evening Standard)
Fer:QPR imekubali kumuuza kiungo wake Mholanzi,Leroy Fer,27,kwenda Swansea City kwa ada ya £4.75m baada ya kuwa na msimu mzuri wakati akiichezea klabu hiyo kwa mkopo.(The Sun)
Ighalo:Watford imekataa ofa ya £37.5m toka Shanghai SIPG ili kumuuza mshambuliaji wake raia wa Nigeria,Odion Ighalo,24.Wakati huohuo klabu hiyo imekamilisha usajili wa mlinzi wa Ubelgiji,Christian Kabasele toka KRC Genk kwa mkataba wa miaka mitano kwa ada ya £5.8m.(Sky sources)
0 comments:
Post a Comment