Madrid,Hispania.
MLINZI wa kushoto wa Real Madrid Marcelo ameamua kutoa bure kabisa medali yake ya ubingwa wa Uefa Champions League aliyoitwaa Jumamosi Mei 28 huko San Siro,Italia kwa klabu yake kuibuka na ushindi wa penati 5-3 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Atletico de Madrid.
Marcelona,28,ambaye katika mchezo wa Jumamosi alicheza dakika zote 120 na kufunga penati moja na kuiwezesha Real Madrid kutwaa ubingwa 11 wa Uefa Champions League amesema anataka kutoa zawadi kwa mashabiki wake kokote kule ulimwenguni.
Amesema "Hakuna kinachoshinda hisia za kuwa wa kwanza.Nataka kushea hisia hizi na wewe,shabiki wangu ambaye ni kila kitu kwangu.
Shea post hii kwenye ukurasa wangu wa Facebook na uniambie kukumbumbu yako bora ya kuwa wa kwanza na mimi nitakupa zawadi ya medali hii na viatu vyangu vya Adidas # X16 boots nilivyochezea kwenye mchezo wa fainali.Mwisho wa zoezi hilo ni Jumamosi Juni 4."Alimaliza Marcelo.
Mpaka sasa Marcelo ana medali mbili za Uefa Champions League,tatu za La Liga na mbili za Copa del Rey tangu atue Real Madrid.
0 comments:
Post a Comment