728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 01, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA BARANI ULAYA JUMATANO YA LEO JUNI 1,2016.


    Asamoah Gyan

    Gyan:Chelsea imeripotiwa kuwa katika mipango ya kumrejesha katika Ligi Kuu ya England Mshambuliaji wa zamani wa Sunderland  Mghana Asamoah Gyan ambaye kwa sasa anaichezea Shanghai SIPG ya China huku akivuna mshahara wa £227,000 kwa wiki.Kabla ya kutua Shanghai SIPG Gyan,30,aliichezea Al Ain ya Abu Dhabi na kuifungia mabao 95 katika michezo 83.(AS)

    Mor:Liverpool imeripotiwa kuwa katika uongozi wa mbio za kutaka kumsajili kiungo kinda wa ushambuliaji wa FC Nordsjaelland Mturuki Emre Mor.Mor,18,ameichezea Nordsjaelland michezo 13,akifunga mabao mawili na kutengeneza mengine mawili.Mbali ya Liverpool vilabu vingine vinavyotaka kumsajili Mor ni Manchester United,Borussia Dortmund na Ajax.(ESPN) 

    Lacazette:Tottenham imeripotiwa kufungua mazungumzo na wakala wa mshambuliaji Alexandre
    Lacazette ili kuangalia uwezekano wa kumsajili nyota huyo wa Olympique Lyonnais mwenye thamani ya £30m.Wakati huohuo Tottenham imeripotiwa kumuweka sokoni mshambuliaji wake Son Heung-Min toka Korea Kusini.(Daily Mirror)

    Rode: Borussia Dortmund imekaribia kujibu mapigo kwa kuondokea na mlinzi wake Mats Hummels baada ya kuripotiwa kuwa karibu kuinasa saini ya kiungo wa Bayern Munich midfielder
    Sebastian Rode.Kwa mujibu wa taarifa toka Ujerumani ni kuwa Rode,25,ataigharimu Borussia Dortmund kitita cha £12m.(Kicker)

    Erkin:Inter Milan imefanikiwa kumsajili mlinzi wa kushoto Mturuki Caner Erkin toka Fenerbahce kwa mkataba wa miaka mitatu.Erkin,27,alijiunga na Fenerbahce mwaka 2010 akitokea CSKA Moscow.Ameichezea Uturuki michezo 46 na kuifungia mabao mawili.

    Lloris:Mlinda mlango wa Tottenham Mfaransa Hugo Lloris ameripotiwa kukataa mkataba mpya wa miaka mitano aliyopewa na klabu hiyo ya Kaskazini mwa jiji la London. Lloris, 29, ana mkataba na Tottenham mpaka mwaka 2019.(Mirror)

    Skrtel:Klabu iliyopanda daraja la Ligi Kuu England,Middlesbrough imeripotiwa kuanza kukiimarisha kikosi chake baada ya kuripotiwa kuandaa kitita cha £6m ili kumsajili mlinzi wa Liverpool Mslovakia Martin Skrtel,31.(The Sun)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA BARANI ULAYA JUMATANO YA LEO JUNI 1,2016. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top