728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 01, 2016

    NONGA AOMBA KUONDOKA YANGA SC ASEMA HATAKI KUITIA HASARA KLABU

    Dar es Salaam,Tanzania.

    Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC, Paul Nonga, ameiandikia barua timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani kutaka
    kuondoka klabuni hapo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

    Akizungumza jana Jumanne,Nonga amedai sababu kubwa ya maamuzi yake hayo ni nafasi finyu ya kucheza aliyonayo katika kikosi cha Yanga
    kutokana ubora walionao wenzake wanaocheza nafasi aichezayo na kusisitiza wanatimiza majukumu yao ipasavyo na kuitendea haki
    nafasi hiyo”.

    JE NI KWELI AMEANDIKA BARUA???

    "Kweli nimeandika barua ya kuomba kuuzwa kwa sababu mkataba wangu unaruhusu kufanya hivyo,lazima tuangalie upande wa pili Yanga wametumia gharama kuninunua, waniuze ili wasipate hasara na sio kunitoa kwa mkopo” Alisema.

    “Nimekwisha peleka barua, bahati nzuri niliwakuta viongozi wote na haya ni maamuzi yangu tukazungumza na mpaka kocha mkuu nimemalizana nae, wameniomba nisubiri mpaka kombe la shirikisho lipite ili taratibu ziendelee".Alimaliza Nonga.

    Nonga alijiunga na Yanga SC mwezi Januari akitokea Mwadui FC ya Shinyanga kabla ya hapo alikuwa akiichezea Mbeya City ya jijini Mbeya.Tangu atue Yanga SC,Nonga amekuwa hapata nafasi mara kwa mara kutokana na kuzidiwa maarifa na washambuliaji wa kigeni wa klabu hiyo Hamis Tambwe na Donald Ndombo Ngoma toka Zimbabwe.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NONGA AOMBA KUONDOKA YANGA SC ASEMA HATAKI KUITIA HASARA KLABU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top