Paris,Ufaransa
Mlinzi mahiri wa kulia wa timu ya taifa ya
Ivory Coast na Klabu ya Paris St-Germain,Serge Aurier ameingia matatani kwa mara nyingine tena baada ya Jumatatu asubuhi kumdunda Askari Polisi mmoja nje ya Klabu moja ya usiku Champs Elysees huko Paris,Ufaransa.
Aurier,22 ambaye alikamatwa na kuzuiliwa kwa muda kabla ya kuachiwa kwa dhamana jana Jumanne anatarajiwa kufikishwa mahakamani Septemba 26 mwaka huu.
Aurier kwa upande wake amewasilisha kesi mahakamani dhidi ya maafisa wa polisi waliomkamata akidai kuwa walimnyanyasa na kumpiga.
Maafisa wakuu wa klabu yake ya Paris Saint Germain wanasubiri mawasiliano rasmi kabla ya kutangaza hatua watakayochukua.
Hii ni mara ya pili kwa Aurier kuingia matatani tangu ajiunge na Paris Saint Germain akitokea Tolousse katika kipindi cha majira yaliyopita ya usajili barani Ulaya kwa ada ya £7m.
Mara ya kwanza ilikuwa ni mwezi Februari pale aliposimamishwa kucheza kwa muda wa wiki sita kwa kosa la kuchapisha/kupost Video kwenye mtandao wake wa kijamii akimtukana Kocha wake Laurent Blanc na wachezaji wenzake Zlatan Ibrahimovic na Muargentina Angel di Maria.
0 comments:
Post a Comment