Sounders,Marekani.
TIMU ya taifa ya Marekani imekuwa ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya Copa America Centenario baada ya alfajiri ya leo kuifunga timu ya taifa ya Ecuador kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza wa robo fainali uliochezwa katika uwanja wa Centurylink Field
Marekeni ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao baada ya Clint Dempsey kufunga dakika ya 12 kisha Gyasi Zardes akaongeza la pili dakika ya 65 akitumia vyema uzembe wa mabeki wa Ecuador walioshindwa kuizuia krosi ya Clint Dempsey.
Dakika ya 74 Michael Arroyo aliifungia Ecuador bao la kufutia machozi kwa mkwaju mkali wa chinichini baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa nahodha Walter Ayovi.
Katika mchezo huo Marekani na Ecuador zililazimika kumaliza pungufu baada ya wachezaji wao Jermain Jones na Antonio Valencia kulimwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.
VIKOSI
United States : Guzan, Besler, Brooks,Cameron, Johnson, Zardes (Birnbaum 90'), Bradley, Jones (red 52'), Bedoya (Zusi 81'), Dempsey (Beckerman 74'),Wood
Ecuador: Dominguez, Ayovi, Erazo,Paredes (Ayovi 82'), Mina, Noboa (Gaibor 62'), Gruezo (Ramirez 72'),
Arroyo, Montero, E.Valencia, A.Valencia (red 52')
RATIBA YA MICHEZO YA ROBO FAINALI NYINGINE
Jumamosi 18 Juni, 2016
03:00 Peru v Colombia
Jumapili 19 Juni, 2016
02:00 Argentina v Venezuela
05:00 Mexico v Chile
0 comments:
Post a Comment