Paris,Ufaransa.
UJERUMANI na Poland zimeshindwa kutambiana baada ya Alhamis usiku kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo mkali wa kundi C wa michuano ya Ulaya maarufu kama Euro uliochezwa katika uwanja wa Stade De France uliokuwa na watazamaji 73,648.
Katika mchezo huo ilishuhudiwa Ujerumani ambao ni mabingwa wa dunia wakishindwa kulenga shuti hata moja langoni kwa Poland katika kipindi chote cha kwanza rekodi ambayo waliiweka mara ya kwanza mwaka 1988 pale walipobanwa vilivyo na Italia na kushindwa kabisa kufurukuta.
Mshambuliaji Arkadiusz Milik angeibuka shujaa kwa upande wa Poland lakini alishindwa kuipa ushindi timu yake baada ya kupoteza nafasi mbili za wazi za kufunga katika kipindi cha pili cha mchezo huo ulioshuhudia tuzo ya mchezaji bora wa mechi ikienda kwa kiungo wa Poland na Sevilla, Grzegorz Krychowiak.
Kwa matokeo hayo Ujerumani imebaki kileleni mwa Kundi C ikiwa na pointi zake nne sawa na Poland lakini zikitofautiana kutokana na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.Nafasi ya tatu imeshikwa na Ireland ya Kaskazini yenye pointi tatu,Ukraine iko mkiani ikiwa haina pointi yoyote.Timu zote zimecheza michezo miwili
VIKOSI
Germany team: Neuer, Hector, Höwedes,Hummels, Khedira, Özil, Draxler, Müller,Boateng, Kroos, Götze
Poland team: Fabianski, Jedrzejczyk, Pazdan,Glik,Piszczek,Grosicki,Maczynski,Krychowiak, Blaszczykowski, Milik,
Lewandowski
0 comments:
Post a Comment