728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 08, 2016

    COPA AMERICA CENTENARIO:COLOMBIA YATINGA ROBO FAINALI,MAREKANI YAAMKA

    Chikago,Marekani.

    TIMU ya taifa ya Colombia imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Copa America Centenario baada ya alfajiri ya leo kuifunga timu ya taifa ya Colombia kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali wa Kundi A uliochezwa katika uwanja wa Rose Bowl,Chicago -Marekani.

    Colombia walianza kujihakikishia ushindi huo dakika ya 9 ya kipindi cha kwanza baada ya Carlos Bacca kufunga baada ya kupokea pasi toka kwa nahodha James Rodriquz .Dakika ya 30 James Rodriguez aliifungia Colombia bao la pili akimalizia pasi ya E Cardona 

    Bao la kufutia machozi la Paraguay limefungwa dakika ya 71 na Victor Ayala kwa mkwaju mkali wa mita 25.Dakika ya 81 Oscar Romero alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.

    Kwa matokeo hayo Colombia imefikisha pointi sita baada ya kushinda michezo yake miwili ya awali hivyo imekuwa timu ya kwanza kutoka Kundi A kufuzu hatua ya robo fainali.

    Katika mchezo wa mapema wa Kundi hilo la A uliochezwa huko Chicago, wenyeji Marekani wameibuka washindi baada ya kuifunga Costa Rica kwa mabao 4-0.Mabao ya Marekani yamefungwa na Clint Dempsey 9',Jermain Jones 37', Bobby Wood 42' na Graham Zusi 87'


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: COPA AMERICA CENTENARIO:COLOMBIA YATINGA ROBO FAINALI,MAREKANI YAAMKA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top