728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 16, 2016

    DHARAU ZAMPONZA MLINZI WA LIVERPOOL AONDOLEWA KIKOSI CHA EURO

    Lovren akiwa uwanjani

    Zagreb, Croatia.

    Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Croatia Ante Cacic amemuacha mlinzi wa Liverpool Dejan Lovren katika kikosi cha wachezaji 27 cha nchi hiyo kinachotarajia kuingia kambini hivi karibuni kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Ulaya (Euro 2016)   

    Hatua hiyo imekuja baada ya mwezi Machi mlinzi huyo mwenye miaka 26 kugoma kufanya warm up katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Hungary baada ya kugundua kuwa jina lake halikuwemo katika kikosi kilichopangwa kuanza katika mchezo huo ulioisha kwa sare ya bao 1-1.

    Akitangaza uamuzi huo Cacic amesema bado milango iko wazi kwa mlinzi huyo kurejea kikosini hapo siku za usoni ikiwa atakuwa amejifunza kuheshimu wachezaji wenzake,benchi la ufundi na wote waliopo katika kikosi cha Croatia.

    Wakati Lovren akitemwa kinda wa FC Barcelona Alen Halilovic,18 aliyekuwa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Sporting Gijon yeye amemjumuisha kwa mara ya kwanza katika kikosi cha wakubwa cha Croatia.

    Wengine waliojumuishwa ni viungo wa Real Madrid Luka Modric na Mateo
    Kovacic,Ivan Rakitic wa FC Barcelona,Mario Mandzukic wa Juventus na nahodha Darijo Srna wa Shakhtar Donetsk.

    KIKOSI KAMILI

    Makipa:Danijel Subasic (Monaco),Lovre Kalinic (Hajduk Split), Ivan Vargic (Rijeka), Dominik Livakovic (NK Zagreb)

    Mabeki : Tin Jedvaj (Bayer Leverkusen),Darijo Srna (Shakhtar Donetsk), Sime Vrsaljko (Sassuolo), Gordon Schildenfeld (Dinamo Zagreb), Vedran Corluka (Lokomotiv Moscow), Domagoj Vida (Dynamo Kiev), Duje Caleta-Car (Red Bull Salzburg), Ivan Strinic (Napoli)

    Viungo: Marko Rog (Dinamo Zagreb),Mateo Kovacic (Real Madrid), Luka Modric (Real Madrid), Marcelo
    Brozovic (Inter), Ivan Rakitic (Barcelona),Milan Badelj (Fiorentina), Domagoj Antolic (Dinamo Zagreb), Ante Coric (Dinamo Zagreb), Ivan Perisic (Inter), Alen Halilovic (Barcelona)

    Washambuliaji : Marko Pjaca (Dinamo Zagreb),Mario Mandzukic (Juventus), Nikola Kalinic (Fiorentina), Duje Cop (Malaga/Dinamo Zagreb), Andrej Kramaric (Hoffenheimm,/Leicester City)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DHARAU ZAMPONZA MLINZI WA LIVERPOOL AONDOLEWA KIKOSI CHA EURO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top