728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, January 06, 2015

    PUYOL,ZUBIZARRETA OUT BARCELONA

    Barcelona, Hispania.
    Baada ya kushindwa kwa rufaa yake huko CAS (FIFA) na kujikuta ikifungiwa kutojihusisha na masuala ya usajili kwa misimu miwili huku ikuanza mwaka 2015 kwa kipigo mambo ndani ya klabu ya Barcelona yamekuwa siyo mambo tena.

    Habari za kuaminika toka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa raisi wa klabu hiyo Jose Maria Batromeu amemtimua kazi mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo Andoni Zubizarreta.
    Zubizarreta ambaye alikuwa ni mlinda mlango wa zamani wa klabu hiyo amehudumu katika nafasi hiyo ya ukurugenzi tangu mwaka 2010.
    Kufuatia timua timua hiyo aliyekuwa mkurugenzi msaidizi wa klabu hiyo Carles Puyol yeye kwa ridhaa yake mwenyewe amejiuzuru nafasi hiyo muda mfupi baada ya bosi wake huyo  kung'olewa madarakani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: PUYOL,ZUBIZARRETA OUT BARCELONA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top