London,England.
Klabu ya Chelsea kupitia wake mkuu Jose Mourinho siku ya leo jumatatu imetoa taarifa za kuondoka kwa mlinda mlango wake Mark Schwarzer anayetimkia klabu nyingine ya ligi kuu ya Leceister City.
Schwazer ambaye aliichezea Chelsea michezo 12 msimu uliopita akiwa ni mlinda mlango chaguo la pili nyuma ya Petr Cech,ameshindwa kuichezea klabu hiyo mchezo wowote msimu huu hasa baada ya kuongezeka kwa mlinda mlango Thibaut Courtois.
Akitoa taarifa za kuondoka kwa Schwarzer,Mourinho amesema "Kwa niaba yangu mwenyewe, wafanyakazi na wachezaji napenda kusema kuwa tutamiss sana Schwarzer na tunamtakia maisha mema huko anakokwenda"
Mark Schwarzer aliyejiunga na Chelsea mwaka 2013 akitokea Fulham anatazamiwa kuwa langoni siku ya jumamosi kuidakia timu yake mpya ya Leceister City itakapovaana na Aston Villa katika mchezo wa ligi kuu kufuatia kuumia kwa mlinda mlango chaguo la kwanza Kasper Schmeichel
0 comments:
Post a Comment