Redio moja mjini hapa imeripoti kuwa mshambuliaji wa klabu ya Rijeka Andrej Kramaric 23 amekubali ofa ya kujiunga na klabu ya Leceister City maarufu kama Foxes.
Leceister City imekubali kutoa kitita cha £9.5m kwa kinda huyo ambaye hapo mwanzo aliripotiwa kuwa karibu kutua klabu ya Chelsea. Habari hizo zinazidi kuripoti kuwa Kramaric amekubali kujiunga na Leceister City baada ya mazungumzo ya siku kadhaa.
Hivi sasa Kramaric yuko England akiwa na wakala wake ambaye ni baba yake Joza Kramaric pamoja na mkurugenzi wa Rijeka Ivan Mance kufanya mazungumzo ya mwisho.
0 comments:
Post a Comment