728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 09, 2017

    Yanga yaichapa Kagera Sugar na kurejea kileleni



    Paul Manjale,Dar Es Salaam.

    YANGA imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kuutetea ubingwa wake iliyoutwaa msimu uliopita baada ya kuifunga Kagera Sugar mabao 2-1 kwenye mchezo wa kiporo wa ligi kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

    Yanga ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Simon Msuva aliyefunga kwa kichwa katika dakika ya 38 akiunganisha kona safi iliyopigwa na Geoffrey Mwashiuya kutoka mashariki mwa uwanja.Hilo limekuwa ni bao la 13 kwa Msuva ligi kuu bara msimu huu.

    Kagera Sugar Mbaraka Yusuph mpira wa juu uliopigwa na Edward Christopher na kumfunga kiufundi kipa wa Yanga leo hii Beno Kakolanya na kufanya mchezo huo uende mapumziko timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1.

    Kipindi cha pili Yanga iliuanza mchezo kwa nguvu na kufanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na Mzambia Obrey Chirwa katika dakika ya 52 akiunganisha krosi safi ya Mnyarwanda Haruna Niyonzima aliyeambana na mpira winga ya kulia na kumzidi ujanja nahodha wa Kagera Sugar,George Kavila.

    Dakika ya 87 Kagera Sugar ilipata pigo baada ya mshambukiaji wake mahiri Mbaraka Yusuph kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumchezea madhambi Kelvin Yondani.

    Ushindi huo umeifanya Yanga ifikishe pointi 62 sawa na wapinzani wao Simba 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Yanga yaichapa Kagera Sugar na kurejea kileleni Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top