728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 09, 2017

    Samatta apishana na tuzo Ubelgiji ni ile ya wachezaji wenye asili ya Afrika


    Brussels, Ubelgiji.

    KIUNGO wa Anderlecht na timu ya taifa ya Ubelgiji,Youri Tielemans (Chini Pichani) akiibusu tuzo ya Ebony Shoe Award baada ya jana Jumatatu usiku kutangazwa mchezaji bora wa mwaka kwa wachezaji wenye asili ya bara la Afrika.

    Tielemans mwenye umri wa miaka 20 na ambaye ana asili ya nchi ya Congo DRC ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda Sofiane Hanni wa Anderlecht, Mbaye Leye wa Zulte Waregem/Senegal,Landry Dimata KV Oostende/Mali na Henry Onyekuru wa Eupen/Nigeria.

    Mtanzania Mbwana Samatta hakuwa kwenye kinyang'anyiro cha wachezaji watano wa mwisho walioingia fainali.





    Tuzo ya Ebony Shoe Award hutolewa kila mwaka na huwa maalumu kwa wachezaji wenye asili ya Afrika wanaocheza ligi kuu ya soka ya nchini Ubelgiji.Kwa mara ya kwanza ilitolewa mwaka 1992 huku Mnigeria,Daniel Amokachi akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuitwaa tuzo hiyo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Samatta apishana na tuzo Ubelgiji ni ile ya wachezaji wenye asili ya Afrika Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top