728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 13, 2017

    Giroud apiga mbili,Arsenal ikiitungua Stoke City 4-1 ligi kuu England


    Stoke,England.

    MABAO mawili ya Mshambuliaji Mfaransa,Olivier Giroud yameipa Arsenal nguvu ya kuchomoza ushindi mnono wa mabao 4-1 ugenini dhidi ya Wagumu,Stoke City kwenye mchezo wa ligi kuu England uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Bet365.

    Mabao mengine ya Arsenal kwenye mchezo wa leo yamefungwa na kiungo Mesut Ozil pamoja na winga Alexis Sanchez ambaye alitolewa baada ya kufunga kutokana na kupata jeraha la nyama za paja.Bao la Stoke City limefungwa na Peter Crouch.

    Ushindi huo umeifanya Arsenal ifikishe pointi 69 baada ya kucheza michezo 36.Pointi moja nyuma ya wanaoshika nafasi ya nne Liverpool wenye pointi 70 na michezo 36.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Giroud apiga mbili,Arsenal ikiitungua Stoke City 4-1 ligi kuu England Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top