London, England.
NYOTA wa kimataifa wa Argentina,Manuel Lanzini (pichani) akishangilia bao lake la dakika ya 65 aliloifungia Westham United jana usiku na kuiwezesha kuifunga Tottenham bao 1-0 katika mchezo mkali wa ligi kuu ya soka nchini England uliochezwa kwenye uwanja wa London Stadium.
Lanzini,26,alifunga bao hilo ambalo ni la nane msimu huu baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mghana,Andrew Ayew na kufumua mkwaju mkali uliomshinda kipa wa Tottenham Mfaransa,Hugo Lloris na kutinga wavuni.
Ushindi huo wa Westham United umetoa mwanya kwa wapinzani wa Tottenham,Chelsea ambao sasa wanahitaji kushinda michezo yao miwili inayofuatia dhidi ya Middlesbrough na Westbrom ili waweze kutawazwa mabingwa wapya wa ligi kuu England msimu wa 2016/17.
0 comments:
Post a Comment