Dar Es Salaam,Tanzania.
AZAM FC imechupa mpaka nafasi ya tatu na kuishuka Kagera Sugar kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka ya Vodacom Tanzania bara baada ya usiku huu kuifunga timu ngumu ya Mbao FC kwa mabao 3-1 katika mchezo mkali uliochezwa kwenye uwanja wa Chamazi Complex uliopo Mbande nje kidogo ya jiji la Dar Es Salaam.
Nahodha John Bocco alianza kuipa uongozi Azam FC baada ya kuifungia bao safi la kuongoza katika dakika ya 12 ya kipindi cha kwanza.Mabao mengine ya Azam FC yamefungwa na Shabani Iddi katika dakika za 53 na 58.Bao la Mbao FC limefungwa na Ndaki Robert katika dakika ya 84.Bao alilofunga Bocco
linamfanya kufikisha mabao tisa msimu huu kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara (VPL) huku Shaaban aliyeingia dakika ya 29 kuchukua nafasi yanaye akiwa
nayo sita kwenye ligi hiyo.
Ushindi huo umeifanya Azam FC ifikishe pointi 49.Pointi moja mbele ya Kagera Sugar yenye pointi 48 ambayo jioni ya leo imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Ruvu Shooting.
0 comments:
Post a Comment