728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 07, 2017

    AS Monaco ikishinda mchezo mmoja tu ubingwa huo


    Bernardo Silva akishangilia bao

    Nancy,Ufaransa.

    AS MONACO sasa inahitaji kushinda mchezo wake mmoja tu ili iweze kutwaa ubingwa wa ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa (Ligue 1) kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2000 hii ni baada ya jana Jumamosi usiku ikiwa ugenini Stade Marcel Picot,Nancy kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji wao AS Nancy Lorraine.

    Mabao ya AS Monaco kwenye mchezo wa jana ambao staa wake Kylain Mbappe alianzia benchi yamefungwa na Tobias Badila aliyejifunga,Bernardo Silva na Thomas Lemar.



    Thomas Lemar wa Monaco kulia akimtoka beki wa Nancy

    Ushindi huo umeifanya AS Monaco ifikishe pointi 86 baada ya kucheza michezo 35.Pointi tatu mbele ya Paris Saint Germain yenye pointi 83 na michezo 36.Ikumbukwe AS Monaco ina wastani wa mabao wa +69 huku wapinzani wao Paris Saint Germain wastani wa mabao wa +51.Hivyo AS Monaco ikiifunga LOSC Lille Jumamosi ijayo kimahesabu itakuwa bingwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AS Monaco ikishinda mchezo mmoja tu ubingwa huo Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top