728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 17, 2017

    50 Cent,Bruno Mars waitwa kunogesha ubingwa wa AS Monaco


    Paris,Ufaransa.

    AS MONACO huenda leo Jumatano ikatawazwa kuwa bingwa mpya wa ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa,Ligue 1 ikiwa tu itashinda ama itatoka sare yoyote ile na Saint-Etienne.

    Jumamosi AS Monaco itashuka tena dimbani kucheza mchezo wake wa mwisho wa kuhitimisha msimu wake wa maajabu mengi na mafanikio.

    Katika kuonyesha kuwa haitaki msimu huu wa maajabu upite kimya kimya,AS Monaco imeandaa pati la nguvu na kumwalika mwanamuziki nguli wa Marekani,Curtis Jackson maarufu kama 50 Cent kwenda kutoa burudani ya kufa mtu kwa wachezaji na wafanyakazi wa timu.


    Pati hiyo itafanyika Jumapili jioni huko Place du Palais mbele ya kasri la Albert II,Mwanamfalme wa Monaco, ambapo mashabiki wa AS Monaco wataruhusiwa kuhudhuria kwa vibali maalumu.

    Wakati huo taarifa zinasema kuwa pia kutakuwa na sapraizi ya mwanamuziki mwingine wa Marekani,Bruno Mars ambaye nae atatua kufanya vitu vyake.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: 50 Cent,Bruno Mars waitwa kunogesha ubingwa wa AS Monaco Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top