Kampala, Uganda.
MLINDA MLANGO namba moja wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini,Denis Onyango ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu ya taifa ya Uganda,Uganda Cranes akichukua mikoba ya mshambuliaji Geoffrey Massa aliyetangaza kustaafu Jumatano iliyopita.
Akizungumzia uteuzi huo kocha mkuu wa Uganda Cranes,Mserbia Milutin ‘Micho’ Sredojevic ameuambia mtandao wa supersport.com kuwa Onyango ameteuliwa kushika wadhifa huo kutokana na kujituma,ukomavu,uongozi,uzoefu pamoja na kuwa na tabia njema.
Micho ameongeza kuwa Onyango ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa wachezaji wa ndani atakuwa akisaidiwa na Hassan Wasswa kuhakikisha kuwa jahazi la Uganda Cranes linafika mbali.
Msimu uliopita Onyango alikuwa shujaa baada ya kuiongoza Mamelodi Sundowns kutwaa mataji matatu makubwa ya klabu bingwa Afrika,Ligi kuu Afrika Kusini na ubingwa wa michuano ya Telkom Cup.
0 comments:
Post a Comment