Dar Es Salaam,Tanzania.
TIMU ya taifa ya vijana ya Tanzania ya wachezaji walio na umri wa chini ya miaka 17,Serengeti Boys leo jioni itashuka kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam kucheza na timu ya taifa ya vijana ya Ghana,Black Starlets katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
Mchezo huo unatarajiwa kuanza mishale ya saa 10:00 jioni utatumiwa na timu hizo mbili kama sehemu ya maandalizi yao kabla ya kuelekea nchini Gabon kwenye michuano ya AFCON ya vijana.
Mchezo huo pia utatumiwa na Serengeti Boys kuwaaga Watanzania kabla ya kwenda nchini Morocco ambako itaweka kambi pamoja na kucheza michezo ya kimataifa ya kujipima nguvu.
Michuano ya AFCON ya vijana imepangwa kuanza kutimua vumbi lake Mei 14 huko nchini Gabon ambapo Serengeti Boys imepangwa kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola.Ghana imepangwa kundi A pamoja na mataifa kama Cameroon na wenyeji Gabon.
0 comments:
Post a Comment