Shinyanga,Tanzania.
TIMU ya Stand United ya Shinyanga maarufu kama Chama la Wana imeanika hadharani mambo mawili makubwa yanayofanya isiwe tishio tena ligi kuu bara kama ilivyokuwa hapo mwanzoni mwa msimu huu.
Akiongea na mwandishi wetu,Mwenyekiti wa timu hiyo Dokta Ellyson Maeja ameyataja mambo hayo kuwa ni ukata wa fedha pamoja na wachezaji kushindwa kushika kwa haraka mifumo/fomesheni za walimu wao.
Maeja amesema ukata wa fedha unatokana na kujitoa kwa aliyekuwa mdhamini wao mkuu kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya ACACIA iliyokuwa inatoa zaidi ya shilingi bilioni moja (1) ya udhamini kwa mwaka.
Ameongeza ukata wa fedha umeifanya Stand United ishindwe kulipa kwa wakati mishahara ya wachezaji wake pamoja na kushindwa kuwapatia mahitaji mengine muhimu.
Jambo la pili ambalo Maeja amelitaja ni wachezaji kushindwa kushika kwa haraka mifumo/fomesheni za walimu wao wapya.Ikumbukwe mwanzoni mwa msimu,Stand United ilikuwa ikifundishwa na Mfaransa Patrick Liewig aliyeikacha timu hiyo baada ya kutokea kutoelewana kati yake na uongozi wa timu hiyo.
Kwa sasa Stand United inashika nafasi ya 9 kwenye msimamo wa ligi kuu bara baada ya kujikusanyia pointi 28 katika michezo 24.
0 comments:
Post a Comment