London, England.
KICHAPO cha mabao 2-1 ilichokipata Chelsea jana Jumamosi jioni kutoka kwa Crystal Palace nyumbani Stamford Blidge siyo kwamba tu kimeipunguza miamba hiyo kasi ya kuusogelea ubingwa wa ligi kuu England msimu huu bali pia kimetibua rekodi binafsi ya kiungo wake,Mhispania Cesc Fabregas.
Ishu iko hivi,Fabregas ambaye alifunga bao pekee la Chelsea kwenye mchezo huo wa jana alikuwa akifikisha bao lake la 43 la ligi kuu England.Idadi hiyo ni pamoja na mabao aliyoyafunga wakati akiichezea Arsenal.
Kati ya mabao hayo 43,Fabregas hakuwahi kupoteza mchezo wowote ule wa ligi kuu England ambao yeye amefunga bao.Kabla alikuwa na rekodi ya kutopoteza mchezo hata mmoja katika michezo 42 ambayo yeye amefunga bao.Katika michezo 43 aliyofunga bao rekodi inasema ameshinda michezo 34,katoka sare michezo 8 na kapoteza mchezo mmoja peke yake.
Mabao ya Crystal Palace yaliyohitimisha safari ndefu ya Fabregas ya kutopoteza mchezo wowote wa ligi kuu ambayo yeye amefunga bao yamefungwa na Wilfried Zaha pamoja na Christian Benteke.
0 comments:
Post a Comment