Paul Manjale
KIUNGO mkabaji wa mabingwa watetezi wa ligi kuu bara,Yanga SC Mzambia Justine Zullu maarufu kama Mkata Umeme anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili na ushee akiuguza jeraha la mguu alilolipata kwenye mchezo wa ligi hiyo jana Jumamosi dhidi ya Azam FC uliochezwa jana Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
Zullu alilazimika kutolewa nje ya dimba katika dakika ya 30 ya kipindi cha kwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Emanuel Martin baada ya kuchanika nyama za ugoko kufuatia kuchezewa rafu mbaya na kiungo wa Azam FC,Himid Mao Mkami.
Zullu alikumbana na balaa hilo wakati akijaribu kupiga shuti kuelekea langoni mwa Azam FC na kulazimika kukimbizwa katika Zahanati ndogo iliyopo ndani ya Uwanja wa Taifa ambapo alishonwa nyuzi tisa ikiwa ni mikakati ya kutibu jeraha hilo.Yanga SC ilishindwa bao 1-0 katika mchezo huo.
Sasa hii ina maana kwamba Zullu ataukosa mchezo wa Jumamosi ijayo wa mkondo wa kwanza wa mtoano wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya MC Alger ya Algeria.Mchezo huo utachezwa April 7 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
0 comments:
Post a Comment