728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, April 04, 2017

    Mbaraka Yusuph Abeid Mchezaji bora mwezi Machi VPL


    Faridi Miraji , Dar es salaam.                           

    Mchezaji wa timu ya Kagera Sugar FC, Mbaraka Yusuph Abeid amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Machi kwa msimu wa 2016/2017.

    Mbaraka aliwashinda wachezaji Abubakar Salum wa Azam FC na Kenny Ally wa Mbeya City kutokana na kuonyesha kiwango cha hali ya juu, hivyo kuisadia timu yake kupata matokeo mazuri.

    Katika mwezi ho ilichezwa raundi moja tu na Mbaraka ambaye alicheza kwa dakika zote 90 aliisaidia timu yake kukusanya pointi zote tatu zilizoifanya timu yake kubaki katika nafasi ya nne (4) katika msimamo wa ligi kwa mwezi huo.

    Katika mchezo huo mmoja, Mshambuliaji huyo alifunga goli moja, na alionyesha nidhamu ya hali ya juu, hivyo kutopata onyo lolote la kadi.Kwa kushinda tuzo hiyo, Mbaraka atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania PLC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Mbaraka Yusuph Abeid Mchezaji bora mwezi Machi VPL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top