728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, February 12, 2017

    Yanga SC yawagonga Wacomoro 5-1 ligi ya mabingwa Afrika

    Moroni,Comoro.

    MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC,leo wameianza vyema safari ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya muda mfupi uliopita wakiwa ugenini huko Moroni,Comoro kuwafunga wenyeji wao Ngaya FC mabao 5-1.

    Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Stade de Moroni (ICR) ilishuhudiwa Yanga SC ikijipatia mabao yake kupitia kwa kiungo wake Mzambia,Justine Zulu,Simon Msuva,Obrey Chirwa,Hamis Tambwe na Thabani Kamusoko.Bao la wenyeji Ngaya FC limefungwa na Said Anifan 

    Aidha katika mchezo huo Yanga SC ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Hamis Tambwe na Haruna Niyonzima na nafasi zao kuchukuliwa na Juma Mahadhi na Emanuel Martin.

    Ushindi huo unaifanya Yanga SC sasa iwe ni kibarua chepesi zaidi siku ya Jumamosi ijayo ambapo itashuka katika uwanja wa taifa Dar Es Salaam kurudiano na Wacomoro hao.

    Ikiwa Yanga itavuka hatua hiyo itakutana na mshindi kati ya Zanaco ya Zambia au APR ya Rwanda ambao katika mchezo wao wa jana uliochezwa huko Lusaka,Zambia walishindwa kufungana.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Yanga SC yawagonga Wacomoro 5-1 ligi ya mabingwa Afrika Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top