Dar Es Salaam,Tanzania
KAMAÑDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam,Simon Sirro amesema kuwa vipimo vya Mkemia Mkuu wa Serikali vimebaini kuwa mfanyabiashara mkubwa ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji anatumia dawa za kulevya.
Akizungumza jana na E-FM, Kamanda Sirro amesema kuwa hali ya Manji ambaye alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha moyo, muda mfupi baada ya kuhojiwa na jeshi hilo inaendelea vizuri na kwamba kesho (leo) atafikishwa mahakamani akikabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa za kulevya.
Kamanda Sirro ameeleza kuwa Manji ameruhusiwa kutoka hospitalini na kwamba amerudishwa katika selo za polisi akisubiri kufikishwa mahakamani.
“[Manji] yuko vizuri na kesho (leo) atapandishwa mahakamani kwa kosa la matumizi ya dawa za kulevya,” kamanda Sirro ameiambia E-FM.
0 comments:
Post a Comment