Madrid,Hispania.
STAA wa Real Madrid,Karim Benzema amempiku Mfaransa mwenzie,Thierry Henry kwenye chati za ufungaji mabao kwenye historia ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya baada ya jana Jumatano kufunga bao lake la 51 kwenye ushindi wa mabao 3-1dhidi ya Napoli.
Katika mchezo huo uliochezwa Santiago Bernabeu,Benzema alifunga bao moja katika dakika ya 18 kwa kichwa akiunganisha krosi ya mlinzi Dani Carvajal na kuwa mbele kwa bao moja zaidi ya Henry mwenye mabao 50 na kuwa Mfaransa mwenye mabao mengi zaidi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Bao hilo pia limemfanya Benzema kushika nafasi ya tano kwenye chati za ufungaji mabao kwenye historia ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya mbele ya magwiji kama Eusebio na Alfredo di Stefano
0 comments:
Post a Comment