728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, August 15, 2016

    UCHAMBUZI:CHELSEA VS WEST HAM - STAMFORD BRIDGE




    Na.Chikoti Cico

    Ni “London Derby” leo usiku (Saa 4:00) katika mechi ya mwisho ya pazia la ligi kuu nchini Uingereza kufunguliwa, ni Conte vs Bilic ukiwa ni mchezo wa kwanza wa mashindano kwa kocha mpya wa Chelsea.

    TAARIFA ZA TIMU:

    CHELSEA.

    Klabu ya Chelsea kuelekea mchezo huo haina mchezaji aliye majeruhi ukiachana na beki Kurt Zouma ambaye aliumia toka msimu uliopita wa ligi. Wakati huo huo huu utakuwa mchezo wa kwanza wa mashindano kwa Michy Batshuayi na N'Golo Kante toka waliposajiliwa.

    WEST HAM.

    Kocha wa West Ham Slaven Bilic kuelekea mchezo huo atawakosa Aaron Cresswell na Manuel Lanzini ambao ni majeruhi, pia kocha huyo amethibitisha kwamba Dimitri Payet bado hayuko fiti kuweza kucheza kwa dakika zote tisini kwenye mchezo huo.

    Wakati huo huo Andre Ayew na Arthur Masuaku ambao wamesajiliwa na West Ham msimu huu kucheza kwao kutategemea kama watakuwa fiti kabla ya mchezo huo dhidi ya Chelsea.





    TAKWIMU KUELEKEA MCHEZO HUO:

    Chelsea hawajafungwa katika michezo 10 iliyopita ya ligi dhidi ya West Ham waliyocheza Stamford Bridge huku wakishinda michezo saba na kutoka sare michezo mitatu na mara ya mwisho kupoteza mchezo wa nyumbani dhidi ya West Ham ni Septemba 2002 walipofungwa kwa magoli 2-3.

    Chelsea ndiyo klabu pekee ndani ya ligi ya primia kunyakua alama nyingi kwa mechi za ufunguzi wa ligi, alama 51.

    Pia Chelsea haijawahi kufungwa mechi ya ufunguzi wa pazia la ligi ya primia iliyochezwa Stamford Bridge katika kila mchezo ndani ya misimu 13 iliyopita huku wakishinda michezo 10 na kutoka sare michezo mitatu.


    Kocha wa Chelsea Antonio Conte amepoteza mchezo mmoja tu kati ya michezo 30 iliyopita ya ligi huku akishinda michezo 27 na kutoka sare michezo miwili.

    Kiungo wa West Ham Dimitri Payet alihusika kwenye magoli 11 (magoli matatu na “assists” nane) ya klabu hiyo katika michezo 12 iliyopita ya ligi aliyocheza ndani ya msimu wa 2015/16.

    Chelsea haijawahi kushinda katika michezo minne iliyopita ya ligi ya primia waliyocheza siku ya Jumatatu, wamefungwa mara mbili na kutoka sare mara mbili.

    Klabu hizi mbili zimekutana mara 105 kwenye ligi ya primia huku Chelsea wakishinda mara 47 nao West Ham wakishinda mara 38 na wametoka sare mara 20.

    VIKOSI VINAWEZA KUWA HIVI:

    Chelsea XI: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Kante, Matic, Willian, Oscar, Hazard, Costa.

    West Ham XI: Adrian, Antonio, Reid, Ogbonna, Byram, Kouyate, Nordtveit, Feghouli, Noble, Payet, Carroll.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UCHAMBUZI:CHELSEA VS WEST HAM - STAMFORD BRIDGE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top