728x90 AdSpace

Monday, August 15, 2016

LUKAS PODOLSKI ASTAAFU SOKA LA KIMATAIFA


Cologne,Ujerumani.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa vilabu vya Arsenal na FC Cologne,Lukas Podolski,leo Jumatatu ametangaza kustaafu kuitumikia timu yake ya taifa ya Ujerumani.

Podolski,31,ametangaza uwamuzi huo mchana huu kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema: 

"Nimemwambia Kocha Joachim Low,sitaichezea tena timu ya taifa ya Ujerumani.Ni uwamuzi mgumu kwangu lakini sina jinsi.Najiweka kando ili nifanye mambo mengine."



Podolski alianza kuichezea Ujerumani mwaka 2004 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Hungary.

Mpaka anastaafu,Poldolski,amefanikiwa kuichezea Ujerumani jumla ya michezo 129 akipachika mabao 48 huku pia akishinda kombe la dunia mara moja hiyo ikiwa ni mwaka 2014 nchini Brazil katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Argentina.

Podolski anakuwa mchezaji wa tano kustaafu kuichezea Ujerumani katika kipindi kisichozidi miaka miwili.Wengine ni Bastian Schweinsteiger,Miloslav Klose,Philipp Lahm na Per Mertesacker.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: LUKAS PODOLSKI ASTAAFU SOKA LA KIMATAIFA Rating: 5 Reviewed By: Unknown