Liverpool, England.
KLABU ya Everton imefanikiwa kumsajili winga wa kimataifa wa Congo DRC,Yannick Bolasie,kutoka klabu ya Crystal Palace kwa ada ya £25m.
Bolasie,27,amejiunga na Everton mkataba wa miaka mitano utakaodumu mpaka mwaka 2021 hii ni baada ya kufaulu zoezi la upimaji wa afya yake lililoanza Jana Jumapili.
Kabla ya kujiunga na Crystal Palace misimu mitatu iliyopita,Bolasie,alikuwa akiichezea klabu ya Bristal City
Bolasie anakuwa mchezaji wa nne kujiunga na Everton katika kipindi hiki cha usajili baada ya Maarten Stekelenburg , Idrissa Gueye na Ashley Williams.
0 comments:
Post a Comment