728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, August 15, 2016

    HENRY AWATAJA WACHEZAJI WAWILI WANAOPASWA KUBORESHA VIWANGO VYAO ARSENAL


    London,England.

    NYOTA wa zamani wa Arsenal,Thierry Henry,amewataja wachezaji Theo Walcott na Alex Oxlade-Chamberlain kuwa wanapaswa kuboresha viwango vyao ili waweze kuisaidia timu hiyo inayousaka ubingwa wa ligi kuu England kwa mwaka wa kumi na mbili sasa bila mafanikio.

    Kupitia katika makala yake iliyochapisha katika gazeti la The Sun la nchini Uingereza,Henry,ameandika:



    Theo Walcott 

    “Nataka kumuona Theo akiwa katika kiwango bora muda wote,iwe winga ama katikati (Ushambuliaji).Nataka kumuona akizivunja vunja timu pinzani kama ambavyo Jamie Vardy, Dimitri Payet na Riyad Mahrez wamefanya msimu uliopita.

    “Lakini baada ya miaka kumi akiwa na Arsenal,bado hatujui ni nafasi ipi hasa inayomfaa.Amekuwa katika kiwango kisichoeleweka.Leo juu,kesho chini.



    Alex Oxlade-Chamberlain

    “Alex Oxlade-Chamberlain ni mchezaji mwingine ambaye anapaswa kuboresha kiwango chake.Amekuwa na matatizo yale yale aliyonayo Theo Walcott.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HENRY AWATAJA WACHEZAJI WAWILI WANAOPASWA KUBORESHA VIWANGO VYAO ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top