728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, August 15, 2016

    TFF YAMWEKA HADHARANI MWAMUZI ATAKAYEZICHEZESHA YANGA,AZAM NGAO YA JAMII JUMATANO.


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    SHIRIKISHO la Soka nchini Tanzani (TFF),limemteua Mwamuzi,Ngole Mwangole,kuchezesha mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii utakaovikutanisha vilabu vya Yanga na Azam siku ya Jumatano.

    Mwangole ambaye ni mwamuzi mwenye beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na mshindi wa tuzo ya Mwamuzi bora wa msimu uliopita,atasaidiwa na Joseph Bulali kutoka Tanga na Frank Komba wa Dar es Salaam huku kamisaa wa mchezo huo akiwa Peter Temu kutoka Arusha.

    Yanga na Azam zitakutana tena keshokutwa (Jumatano) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,baada ya msimu uliopita Yanga kutwaa ngao hiyo kwa mikwaju ya penalti 8-7 kufuatia kutoka suluhu ndani ya dakika 90.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TFF YAMWEKA HADHARANI MWAMUZI ATAKAYEZICHEZESHA YANGA,AZAM NGAO YA JAMII JUMATANO. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top