Salvador, Brazil.
NIGERIA imekuwa timu ya pili kwa upande wa soka la wanaume kutinga nusu fainali ya michuano ya Olimpiki baada ya Jumamosi Usiku kuchomoza na ushindi safi wa mabao 2-0 dhidi ya Denmark katika mchezo mkali wa robo fainali uliochezwa katika uwanja wa Fonte NovaSalvador huko Salvador.
Mabao ya Nigeria katika mchezo huo yamefungwa na Nahodha,John Obi Mikel,dakika ya 15 akimalizia krosi safi ya Imoh Ezekiel.Bao la pili limefungwa kwa kichwa na Umar Aminu dakika ya 59 ya mchezo akiunganisha kona safi ya Nahodha,John Obi Mikel.
Kwa matokeo hayo sasa Nigeria itavaana na Ujerimani katika mchezo wa nusu fainali utakaochezwa siku ya Jumatano huko Corinthians Arena, Sao Paulo.
Katika mchezo wa mapema Ujerumani iliitandika Ureno kwa jumla ya mabao 4-0 katika mchezo safi uliochezwa katika uwanja wa Estadio Nacional Mane Garrincha huko Brasilia.
Kikosi cha Nigeria kiliwakilishwa na Daniel, Abdullahi, Troost-Ekong,Seth,Amuzie, Okechukwu, Mohammed, Obi (C),A. Umar, S. Umar, Ezekiel.
0 comments:
Post a Comment