Manchester, England.
BAO la kujifunga la dakika ya 87 la Mlinzi,Paddy McNair,limeipa Manchester City ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Sunderland katika mchezo Mkali ulioisha hivi punde katika uwanja wa Etihad,Manchester.
Wenyeji Manchester City ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao baada ya Mshambuliaji wake Sergio Aguero kufunga kwa mkwaju wa penati dakika ya 4 ya kipindi cha kwanza.
Dakika ya 71 Jermain Defoe aliisawazishia Sunderland bao kabla ya dakika ya 87 Paddy McNair kujifunga na kuifanya Manchester City itoke uwanjani ikiwa kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-1.
0 comments:
Post a Comment