Brasilia, Brazil.
UJERUMANI U23 imekuwa timu ya kwanza ya soka kutinga nusu fainali ya michuano ya Olimpiki kwa wanaume baada ya usiku huu kuifunga Ureno U23 kwa mabao 4-0 katika mchezo safi wa robo fainali uliochezwa katika uwanja wa Estádio Nacional Mané Garrincha,Brasilia.
Mabao yaliyoipa Ujerumani ushindi huo mnono siku ya leo yamefungwa na Serge Gnabry 45',Matthias Ginter 57', Davie Selke 75' na Max Meyer 87'.
Mchezo mwingine wa robo fainali utakuwa hapo baadae ambapo wawakilishi pekee wa Afrika katika hatua hiyo Nigeria watashuka dimbani kucheza na Denmark katika mchezo unaotarajiwa kuwa utakuwa wa vuta nikuvute.
0 comments:
Post a Comment