728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, August 14, 2016

    HATIMAYE LINEKER ATIMIZA AHADI AENDESHA SHOW YA TV AKIWA NA NGUO YA NDANI PEKEE


    London, England.

    AHADI ni deni na ni lazima lilipwe.Hiki ndicho alichokifanya Legendi wa zamani wa Leceister City,Gary Lineker,baada ya Jana Jumamosi kuendesha Show kupitia BBC akiwa katika nguo zake za ndani (Underpants)

    Kisa Nini?

    Msimu uliopita Lineker,55, alitoa ahadi kuwa kama klabu yake ya zamani ya Leceister City ingetwaa ubingwa wa ligi kuu England basi angeuanza msimu mpya wa Show yake ya "Match Of The Day" inayorushwa na BBC akiwa katika nguo za ndani pekee na hicho amekidhihirisha Jana Jumamosi baada ya kutangaza kwa takribani dakika 30 nzima akiwa nusu mtupu.



    Kama ambavyo wapenzi wengi wa soka duniani walivyoshindwa kuamini kuwa Leceister City ingetwaa ubingwa wa ligi kuu England basi ndivyo ilivyokuwa kwa Lineker aliyewahi kuichezea pia klabu ya Tottenham.

    Lineker anakuwa mchezaji wa pili kutimiza ahadi yake baada ya Ahmed Mido wa Misri ambaye alinyolewa kipara watu wakishuhudia Live kupitia TV mapema mwezi Mei.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HATIMAYE LINEKER ATIMIZA AHADI AENDESHA SHOW YA TV AKIWA NA NGUO YA NDANI PEKEE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top