Cairo,Misri.
KOCHA Martin Jol amejiuzulu kuifundisha klabu ya Al Ahly ya Misri ikiwa ni miezi sita tu tangu apewe kibarua hicho.
Jol,60,aliyewahi kuvinoa vilabu vya Ulaya vya Ajax,Hamburg na Tottenham amefikia uwamuzi huo baada ya kushindwa kuipeleka timu hiyo katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika.
Al Ahly ilishindwa kuingia hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Afrika baada ya Ijumaa iliyopita kulazimishwa sare ya mabao 2-2 nyumbani na Zesco United ya Zambia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika mtandao rasmi wa klabu hiyo imesema Al Ahly imekubali kuvunja mkataba na Jol baada ya kocha huyo raia wa Uholanzi kuomba kusitisha kibarua chake na nafasi yake itakuchuliwa na aliyekuwa msaidizi wake,Ossama Orabi.
Akiwa na Al Ahly,Jol,aliiwezesha miamba hiyo ya jiji la Cairo kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Misri mwezi Julai huku Agosti 8 akishindwa kutwaa ubingwa wa FA CUP baada ya kufungwa mabao 3-1 na wapinzani wao wa jadi Zamalek katika mchezo wa fainali.
0 comments:
Post a Comment