728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, August 19, 2016

    HATIMAYE LIVERPOOL YAPATA MNUNUZI WA CHRISTIAN BENTEKE


    Liverpool,Uingereza.

    HATIMAYE Liverpool imeridhia kumuuza mshambuliaji wake raia wa Ubelgiji,Christian Benteke,kwenda Crystal Palace hii ni baada ya klabu hiyo ya London kukubali kutoa dau la £32m.

    Kwa mujibu wa habari zilizochapishwa katika mitandao ya vilabu vyote viwili,Crystal Palace, inamsajili Benteke,25,kwa ada ya awali ya £27m ambayo baadae itaongezea kwa £5m zaidi.

    Benteke alijiunga na Liverpool msimu uliopita akitokea Aston Villa kwa ada ya £32.5m lakini kutokana na kuwa majeruhi wa mara kwa mara alijikuta akishindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo mbele ya Divock Origi na Roberto Firmino.

    Benteke anaiacha Liverpool akiwa ameifungia mabao 9 katika michezo 14 ya ligi kuu aliyoanza katika kikosi cha kwanza.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HATIMAYE LIVERPOOL YAPATA MNUNUZI WA CHRISTIAN BENTEKE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top