Liverpool, England.
BAADA ya jana Jumatano kumuuza aliyekuwa mlinzi wake mahiri,John Stones,kwa dau la £47.5m jioni ya leo Everton imemsajili mlinzi wa kimataifa wa Wales,Ashley Williams,kutoka klabu ya Swansea City.
Williams,31,ambaye alikuwa nahodha wa kikosi cha Wales kilichofika nusu fainali ya michuano ya Ulaya (Euro 2016) amesaini kandarasi ya miaka mitatu kuichezea Everton kwa ada ya uhamisho ya £12m.
Akifanya mahojiano baada ya kukamilisha usajili huo Williams amesema:
"Nimekuwa na miaka minane mizuri Swansea City.Baada ya hapo nadhani changamoto mpya ndicho kitu nilichohitaji.Nimefurahi kujiunga na Everton.Everton ni klabu kubwa yenye Kocha mzuri"
Williams alijiunga na Swansea City mwaka 2008 akitokea klabu ndogo ya Stockport County kwa ada ya uhamisho ya £400,000.
Akiwa na Swansea City,Williams,aliiwezesha klabu hiyo ya Wales mwaka 2011 kupanda daraja mpaka ligi kuu na miaka miwili baadae alikuwa sehemu ya kikosi hicho kilichotwaa ubingwa wa kombe la FA.