Salvador,Brazil.
BAADA ya kushindwa kupata ushindi wala kufunga bao lolote katika michezo yake miwili ya awali,Brazil,imeamka na kuishindilia Dermark kwa jumla ya mabao 4-0 katika mchezo safi wa kundi A wa michuano ya Olimpiki kwa wanaume uliochezwa Alfajiri katika Uwanja wa Fonte Nove Arena huko Salvador, Brazil.
Mabao yaliyomaliza mwanzo mbaya kwa wenyeji Brazil yamefungwa na Luan,Gabriel Barbosa aliyefunga mara mbili na Gabriel Jesus aliyefunga bao moja
Ushindi huo umeifanya Brazil ifikishe alama tano na kufanya imalize ikiwa kileleni mwa kundi A na hivyo kutinga robo fainaili ambapo Jumamosi itacheza na mshindi wa pili wa kundi B ambaye ni Colombia.
Licha ya kupokea kichapo hicho kikubwa bado Denmark imefanikiwa kutinga robo fainali na itakutana na Nigeria ambao ni vinara wa kundi B.
Katika mchezo mwingine wa kundi A uliochezwa Alfajiri ya leo,Iraq na Afrika Kusini zimeshindwa kutambia baada ya kutoka sare ya 1-1 matokeo ambayo yanazifungasha timu hizo virago na kurejea nyumbani.
0 comments:
Post a Comment