728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, August 11, 2016

    DONALD NGOMA MCHEZAJI BORA WA GOAL WA MSIMU LIGI KUU BARA

    Dar Es Salaam,Tanzania.

    Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma ameibuka kuwa mshindi wa tuzo ya Goal ya msimu Ligi Kuu Bara kufuatia mchango wake mkubwa katika kampeni za michuano mbalimbali akiwa na wakali wa Jangwani.

    Mshambuliaji huyo wa Yanga amewatupa kwa mbali wachezaji wenzake waliokuwa wakiwania tuzo hiyo Ibrahim Ajibu,Thabani Kamusoko, Juma Abdul, Aishi Manula, Shomari Kapombe, Amissi Tambwe, Farid Mussa, Shiza Kichuya na Juma Jeremiah.

    Ngoma alifunga mabao 17 Ligi Kuu Bara msimu uliopita vijana hao wa Hans van der Pluijm walipoibuka mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

    Ibrahim Ajibu, Amissi Tambwe na Juma Abdul walitajwa kuwania tuzo hiyo baada ya kuonyesha uwezo mkubwa na mchango kwa timu zao lakini wamejikuta wakitupwa mbali kabisa na Mzimbabwe huyo.

    Donald Ngoma meshinda kwa 44% ya kura zote zilizopigwa akifuatiwa na Ibrahim Ajib wa Simba 20%, Amissi Tambwe akishika nafasi ya tatu kwa 9% na Juma Abdul aliyetwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu akiambulia asilimia 8 tu.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DONALD NGOMA MCHEZAJI BORA WA GOAL WA MSIMU LIGI KUU BARA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top