728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, August 11, 2016

    WAALGERIA WAPEWA RUNGU KUZIAMUA TAIFA STARS,NIGERIA AFCON


    Cairo,Misri.

    SHIRIKISHO la Soka Afrika,CAF,leo limemtangaza Mwamuzi,Mehdi Abid Charef,kutoka nchini Algeria kuwa ndiye atakayechezesha mchezo wa marudiano wa kundi G wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya AFCON kati ya wenyeji  Nigeria dhidi ya wageni Tanzania (Taifa Stars).

    Mbali ya Charef waamuzi wengine waliopewa jukumu la kuchezesha mchezo huo ambao nao ni kutoka nchini Algeria ni Abdelhak Etchiali na Ahmed Tamen.Mustapha Ghorbal atakuwa mwamuzi wa akiba.Kamisaa/Kamishna wa mchezo huo atakuwa Inyangi Bokinda kutoka nchini Congo DRC.

    Tanzania na Nigeria zinatarajiwa kurudiana Septemba 3,2016 katika uwanja wa Adokiye Amiesiamaka ulioko katika mji wa Port Harcourt.Mchezo huo utakuwa ni wa kukamilisha ratiba kwani tayari timu zote mbili zimeshindwa kufuzu baada ya kumaliza nyuma ya vinara Misri.

    Katika mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar Es Salaam miezi kadhaa iliyopita timu hizo zilishindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bila kufungana.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WAALGERIA WAPEWA RUNGU KUZIAMUA TAIFA STARS,NIGERIA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top