728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, August 11, 2016

    DROO YA RAUNDI YA PILI EFL:CHELSEA,LIVERPOOL ZAPANGWA NA VIBONDE


    London,England.

    DROO ya michuano ya kombe la ligi EFL zamani Capital One imefanyika Jana Jumatano Usiku.Katika Droo hiyo vigogo vya Chelsea na Liverpool vimepangwa kufungua dimba kwa kucheza na vilabu vya madaraja ya chini.

    Chelsea itaanza kuusaka ubingwa wa michuano hiyo ambayo msimu huu imekosa mdhamini baada ya Capital One kumaliza mkataba kwa kuvaana na mshindi katika ya ndugu wawili Bristol Rovers ama Bristol City.

    Liverpool wao watakuwa wageni wa Burton Albion katika dimba la Pirelli Stadium.Michezo yote ya raundi ya pili itachezwa kati ya Agosti 22 na 23 na timu zitakazoshinda zitaingia raundi ya tatu na kujumuisha na vilabu vingine ambavyo havipo katika raundi ya pili.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DROO YA RAUNDI YA PILI EFL:CHELSEA,LIVERPOOL ZAPANGWA NA VIBONDE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top