728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, August 11, 2016

    KAZI KAZI:SUNDERLAND YASAJILI WAWILI KUTOKA MANCHESTER UNITED


    Sunderland,England.

    MENEJA mpya wa Sunderland,David Moyes,ameendelea na mikakati ya kukiimarisha kikosi chake tayari kwa msimu mpya wa ligi hii ni baada ya hivi punde kukamilisha usajili wa walinzi wawili Paddy McNair na Donald Love kutoka Manchester United kwa ada ya jumla ya £5.5m.

    Walinzi hao ambao wote wana umri wa miaka 21 kila mmoja,wamesaini mkataba wa miaka minne minne baada ya kufaulu zoezi la upimaji wa afya zao.



    McNair anayetokea Ireland Kaskazini amenunuliwa kwa ada ya £4.5m huku Love anayetokea Scotland akinunuliwa kwa ada ya £1m.

    McNair ameiacha Manchester United baada ya kuichezea jumla ya michezo 27 akiwa na kikosi cha kwanza.Msimu uliopita alifanikiwa kuanza katika michezo mitatu pekee tofauti na msimu wa 2014-15 ambapo alifanikiwa kuanza katika michezo 12.

    Love alifanikiwa kuingia katika kikosi cha kwanza mara mbili pekee na msimu uliopita alikuwa akiichezea Wigan Athletic kwa mkopo.

    Huo ni usajili wa pili na wa tatu kufanywa na Moyes tangu apewe mikoba ya kuinoa Sunderland mwezi uliopita.Wa kwanza alikuwa ni mlinzi Papy Djiboloudji kutoka Chelsea kwa ada ya £8m.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KAZI KAZI:SUNDERLAND YASAJILI WAWILI KUTOKA MANCHESTER UNITED Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top