Brasilia,Brazil.
BRAZIL imeanza kichovu harakati zake za kuisaka medali yake ya kwanza ya michuano ya Olyimpiki kwa upande wa soka la wanaume baada ya Alhamis Usiku kulazimisha sare ya bila kufungana na Afrika Kusini katika mchezo mkali wa kundi A uliochezwa katika Uwanja wa Mane Garrincha Stadium,Brasilia hali iliyofanya mashabiki wake kuizomea.
Licha ya kuwa na safu kali ya ushambuliaji ikiongozwa na nahodha wake Neymar Jr,Gabriel Jesus na Gabriel Barbosa Gabigol ,Brazil imejikuta ikikosa mbinu za kuugusa wavu wa Afrika Kusini iliyolazimika kumaliza mchezo ikiwa pungufu baada ya mlinzi wake Mothobi Mvala kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 59 kwa mchezo mbaya.
Matokeo Mengine
Kundi A
Iraq 0-0 Denmark
Kundi B
Colombia 2-2 Sweden
Kundi C
Mexico 2 -2 Ujerumani
Kundi D
Ureno 2-0 Argentina
Ratiba ijayo
Jumapili
Brazil v Iraq
Afrika Kusini v Denmark .
0 comments:
Post a Comment