Etobo
Manaus,Brazil.
NIGERIA imeianza vyema michuano ya soka ya Olyimpiki kwa upande wa wanaume baada ya Alfajiri ya leo kuifunga Japan kwa jumla ya mabao 5-4 katika mchezo mkali wa kundi B uliochezwa katika Uwanja wa Amazonia ulioko Manaus,Brazil.
Mabao ya Nigeria katika mchezo huo yamefungwa na Sadiq Umar 6' na Oghenakaro Etobo na aliyefunga mara nne 10', 42', 51', 66'.
Japan wamepata mabao yao kupitia kwa Shinzo Koroki 9',Takumi Minamino 11',Takuma Asano 70' na Musashi Suzuki 90'
Nigeria na Japan zitarejea tena dimbani siku ya Jumapili katika uwanja huohuo wa Amazonia kuvaana na Sweden na Colombia.
Katika mchezo wa mapema Sweden na Colombia zilikwenda sare ya kufungana mabao 2-2.
Kwa upande wa Sweden wafungaji walikuwa Mikael Ishak (43) na Astrit Ajdarevic (62) huku Colombia ikipata mabao yake kupitia kwa Teofilo Gutierrez (17) na Dorlan Pablon (75-pen).
0 comments:
Post a Comment