728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, August 05, 2016

    SAMATTA NA GENK YAKE MAMBO YAZIDI KUWANYOOKEA EUROPA LIGI WASHINDA UGENINI,WAKARIBIA MAKUNDI

    Cork City,Ireland.

    NDOTO ya Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania,Mbwana Ally Samatta,kucheza hatua ya Makundi ya Michuano ya Europa Ligi imebakiza hatua chache itimie hii ni baada ya usiku huu klabu yake KRC Genk kupata ushindi safi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Cork City katika mchezo mkali wa marudiano wa hatua ya tatu ya mtoano wa michuano hiyo uliochezwa katika Uwanja wa Turner's Cross,Cork-Ireland.

    Katika mchezo huo ambao,Samatta,alicheza kwa dakika 77 kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Bryan Heynen,ilishuhudiwa KRC Genk ikipata mabao yake yote kipindi cha kwanza kupitia kwa nahodha Thomas Buffel dakika ya 13 na Sebastien Dewaest dakika ya 40.Bao la Cork City limefungwa na Alan Bennett dakika ya 63 ya kipindi cha pili.

    Kwa matokeo hayo KRC Genk imefuzu hatua ya mwisho ya mchujo kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1.Katika mchezo wa kwanza ulichezwa katika dimba la Luminus Arena huko Genk Ubelgiji,KRC Genk iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Leon Bailey.

    Droo ya hatua ya mwisho ya mchujo inatarajiwa kupangwa kesho Ijumaa Agosti 5 na mechi za kwanza zitachezwa Agosti 18 wakati zile za marudiano zikichezwa Agosti 25.

    VIKOSI

    Cork City: Mark McNulty; Michael McSweeney (Mark O’Sullivan, HT), Alan Bennett, Kenny Browne, Kevin O’Connor;Greg Bolger (c); Stephen Dooley, Garry Buckley, Gearoid Morrissey (Danny Morrissey, HT), Steven Beattie; Sean Maguire (Karl Sheppard, 56).

    KRC Genk: Marco Bizot; Sandy Walsh,Sebastien Dewaest, Dries Wouters, Jere Uronen; Thomas Buffel (Holly Tshimanga,84), Wilfred Ndidi, Alejandro Pozuelo, Leon Bailey (Leandro Trossard, 65); Ally Samatta (Bryan Heynen, 77), Neeskens Kebano.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SAMATTA NA GENK YAKE MAMBO YAZIDI KUWANYOOKEA EUROPA LIGI WASHINDA UGENINI,WAKARIBIA MAKUNDI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top