London, England.
ARSENAL imefanya usajili wa nne hii ni baada ya leo Jumatano kumsajili kiungo na nahodha wa timu ya taifa ya Nigeria ya U-20 ,Kelechi Nwakali,kutoka katika kituo cha michezo cha Diamond Football Academy.
Nwakali,18,ambaye anawakilishwa na nyota wa zamani wa Arsenal,Nwankwo Kanu,kama wakala wake amesaini mkataba wa miaka mitano utakaodumu mpaka mwaka 2021 baada ya Arsenal kutoa kitita cha £3m.
Mwezi Januari mwaka huu Arsenal ilimfanyia majaribio,Nwakali,na baada ya kufuzu mara moja ilianza mazungumzo na kituo cha Diamond Football Academy kilichokuwa kinammiliki.
Mwaka 2015,Nwakali,alikuwa gumzo duniani baada ya kukiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria cha wachezaji waliochini ya miaka 17 kutwaa Kombe la Dunia la vijana huku yeye akitangazwa mchezaji bora wa michuano hiyo iliyofanyika nchini Chile.
Mbali ya Arsenal inasemekana pia vilabu vya Manchester City na Chelsea navyo viliripotiwa kuitaka saini ya kiungo huyo ambaye kiuchezaji anafananishwa na kiungo wa Ivory Coast,Yaya Toure.
Nwakali anakuwa mchezaji wa nne kujiunga na Arsenal baada ya Granit Xhaka,Takuna Asano na Rob Holding.
0 comments:
Post a Comment